sw_tn/2co/01/intro.md

1.5 KiB

2 Wakorintho 01 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Kifungu cha kwanza kinaonyesha njia ya kawaida ya kuanzisha barua katika inchi ya kale ya Mashariki ya Karibu.

Dhana maalum

Uadilifu wa Paulo

Watu walikuwa wanamkosoa Paulo na kusema kuwa yeye hakuwa wa dhati. Anawakemea kwa kuelezea nia zake kwa kile alichokifanya.

Faraja

Faraja ni neno kuu ya sura hii. Roho Mtakatifu huwafariji Wakristo. Pengine Wakorintho walikuwa wanasumbuliwa na walihitaji kufarijiwa.

Mifano muhimu za matamshi katika sura hii

Swali la uhuishaji

Paulo anatumia maswali mawili ya uhuishaji ili kujitetea dhidi ya madai yasiyokuwa ya kweli. (See: rc://en/ta/man/translate/figs-rquestion)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Sisi

Paulo anatumia neno "sisi". Hii inawezekana kuwakilisha Timotheo na yeye mwenyewe. Inaweza pia kuwajumuisha watu wengine.

Dhamana

Paulo anasema kuwa Roho Mtakatifu ni dhamana, ambayo ina maana ya ahadi au malipo ya kwanza, ya maisha ya Milele ya Mkristo. Wakristo wanaokolewa salama. Lakini hawatapata ahadi zote za Mungu mpaka baada ya kufa. Roho Mtakatifu ni dhamana ya kibinafsi kwamba haya yatafanyika. Wazo hili linatoka kwa tamko la biashara. Mtu hutoa kitu cha bei kubwa kwa mtu mwingine kama "dhamana" kwamba watalipa pesa zote baadaye. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/eternity]] and [[rc://en/tw/dict/bible/kt/save)

| >>