sw_tn/2co/front/intro.md

5.7 KiB

Utangulizi wa 2 Wakorintho

Sehemu ya 1: Utangulizi wa Ujumla

Maelezo ya Kitabu cha 2 Wakorintho

  1. Paulo anashukuru Mungu kwa Wakristo wa Korintho (1:1-11)
  2. Paulo anaelezea mwenendo wake na huduma yake (1:12-7:16) 1.Paulo anaongea kuhusu kuchangia fedha kwa kanisa la Yerusalemu (8:1-9:15)
  3. Paulo anatetea mamlaka yake kama mtume (10:1-13:10)
  4. Paulo anatoa salamu za mwisho na himizo (13:11-14)

Nani aliandika Kitabu cha 2 Wakorintho?

Paulo aliandika 1 Wakorintho. Paulo alitoka mji wa Tarso. Alikuwa anajulikana kama Sauli katika maisha yake ya awali. Kabla ya kuwa Mkristo, Paulo alikuwa Mfarisayo. Aliwatesa Wakristo. Baada ya kuwa Mkristo, alisafiri mara kadhaa katika Ufalme wa Roma akiwaambia watu kuhusu Yesu.

Paulo alianzisha kanisa lililokutana huko Korintho. Alikuwa akiishi katika mji wa Efeso wakati aliandika barua hii.

Je, kitabu cha 2 Wakorintho kinahusu nini?

Katika 2 Wakorintho, Paulo aliendelea kuandika juu ya migogoro kati ya Wakristo katika jiji la Korintho. Ni wazi katika barua hii kwamba Wakorintho walikuwa wametii maelekezo yake ya awali kwao. Katika 2 Wakorintho, Paulo aliwahimiza kuishi kwa njia ambayo ingeweza kumpendeza Mungu.

Paulo pia aliwaandikia kuwahakikishia kwamba Yesu Kristo alimtuma awe mtume kuhubiri Injili. Paulo alitaka waelewe jambo hilo, kwa sababu kundi la Wakristo wa Kiyahudi walipinga kile alichokifanya. Walisema Paulo hakutumwa na Mungu na alikuwa akifundisha ujumbe wa uwongo. Kundi hili la Wakristo Wayahudi walitaka Wakristo wasio Wayahudi kutii sheria ya Musa.

Je, kichwa cha kitabu hiki kinapaswa kutafsiriwaje?

Watafsiri wanaweza kuchagua kuita kitabu hiki kwa kichwa chake cha jadi, "Wakorintho wa Pili." Au wanaweza kuchagua kichwa wazi, kama "Barua ya pili ya Paulo kwa Kanisa la Korintho." (See: rc://en/ta/man/translate/translate-names)

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za Kidini na za Kitamaduni

Mji wa Korintho ulikuwaje?

Korintho ilikuwa mji mkuu katika Ugiriki wa kale. Kwa sababu ulikuwa karibu na Bahari ya Mediterane, wasafiri wengi na wafanyabiashara walikuja kununua na kuuza bidhaa huko. Hii ilisababisha mji kuwa na watu kutoka tamaduni nyingi tofauti. Mji huo ulijulikana kwa kuwa na watu waliokuwa wameishi katika njia za uasherati. Watu waliabudu Afrodito, mungu wa kike wa upendo wa Kigirik. Kama sehemu ya sherehe za kuheshimu Afrodito, waabudu wake walifanya ngono na makahaba wa hekalu.

Paulo alimaanisha nini kwa "mitume wa uongo" (11:13)?

Hawa walikuwa Wakristo wa Wayahudi. Walifundisha kwamba Wakristo wa Mataifa walipaswa kutii sheria ya Musa ili kufuata Kristo. Waongozi wa Kikristo walikutana huko Yerusalemu na kuamua juu ya jambo hilo (Angalia: Matendo 15). Lakini, ni wazi kwamba kulikuwa tena makundi kadhaa ambayo walikataa kile kilichoamuriwa na waongozi wa Yerusalemu.

Sehemu ya 3: Masuala muhimu ya Tafsiri

"Umoja na wingi wa neno "you"

Katika kitabu hiki, neno "mimi" linamaanisha Paulo. Pia, neno "nyinyi" ni karibu kila mara kwa wingi na linamaanisha waumini huko Korintho. Lakini, kuna tofauti mbili kati ya misitari ya 6:2 na 12:9. (See: rc://en/ta/man/translate/figs-exclusive]] and [[rc://en/ta/man/translate/figs-you)

Je, mawazo ya "takatifu" na "kutakasa" yanawakilishwaje katika 2 Wakorintho kwenye ULB?

Maandiko hutumia maneno kama hayo ili kuonyesha moja ya mawazo mbalimbali. Kwa sababu hii, mara nyingi ni vigumu kwa watafsiri kuyawakilisha vizuri katika tafsiri zao. Katika kutafsiri kwa Kiingereza, ULB inatumia kanuni zifuatazo:

  • Mara na mara maana ya kifungu inaashiria utakatifu wa maadili. Hasa ni muhimu kuelewa injili kuwa ni kweli kwamba Mungu anawaona Wakristo kuwa wasio na dhambi kwa sababu wameungana na Yesu Kristo. Ukweli mwingine unaohusiana na haya ni kwamba Mungu ni mkamilifu na hana hatia. Ukweli wa tatu ni kwamba Wakristo wanapaswa kujiendesha kwa njia isiyo na hatia katika maisha yao. Katika hali hizi, ULB inatumia "takatifu," "Mungu mtakatifu," "watakatifu," au "watu watakatifu."

  • Mara nyingi katika kitabo cha 2 Wakorinto,maana ya maneno ni umbukumbu rahisi ya Wakristo bila kutaja jukumu yao fulani. Katika nyakati hizi, ULB inatumia "mwamini" au "waumini." (Angalia: 1:1, 8:4; 9:1, 12; 13:13)

  • Wakati mwingine maana katika kifungu hiki inaashiria mtu au kitu kilichowekewa Mungu peke yake. Katika matukio haya, ULB inatumia "kuwekwa kando," "kujitolea," "iliyohifadhiwa," au "kutakaswa."

Mara nyingi UDB husaidia watafsiri kufikiri juu ya jinsi ya kuwakilisha mawazo haya katika tafsiri zao wenyewe.

Paulo alimaanisha nini kwa maneno "katika Kristo" na "katika Bwana"?

Maneno haya hutokea katika 1:19, 20; 2:12, 17; 3:14; 5:17, 19, 21; 10:17; 12:2, 19; na 13:4. Paulo alijaribu kueleza wazo la muungano wa karibu kati ya Kristo na waumini. Lakini, mara nyingi alitaka kuelezea maan nyingine pia kwa wakati huo huo. Kwa mfano, angalia, "Mlango ulifunguliwa kwangu katika Bwana," (2:12) ambako Paulo alinamaanisha kuwa mlango ulifunguliwa kwa Paulo naye Bwana.

Tafadhali angalia utangulizi wa Kitabu cha Warumi kwa maelezo zaidi juu ya aina hii ya kujieleza.

"Kuwa kiumbe kipya" katika Kristo" kuna maana gani (5:17)

Ujumbe wa Paulo ni kwamba Mungu hufanya Wakristo kuwa sehemu ya "ulimwengu mpya" wakati mtu anaamini Kristo. Mungu anatoa ulimwengu mpya wa utakatifu, amani, na furaha. Katika ulimwengu huu mpya, waumini wana asili mpya ambayo wamepewa na Roho Mtakatifu. Watafsiri wangejaribu kuelezea wazo hili.

Je, kuna masuala gani muhimu katika Kitabu cha 2 Wakorintho?

  • "na katika upendo wenu kwetu" (8:7). Matoleo mengi, na ULB na UDB pia, husoma namuna hii. Hata hivyo, matoleo mengine mengi yanasoma, "na katika upendo wetu kwa ajili yenu." Kuna ushahidi wenye nguvu kwamba kila somo ni la asili. Watafsiri wanapaswa kufuata somo iliyopendekezwa na matoleo mengine katika eneo lao.

(See: rc://en/ta/man/jit/translate-textvariants)