sw_tn/2co/01/01.md

1008 B

Sentensi unganishi

Baada ya salamu za Paulo kwa Kanisa la Korintho, anaandika kuhusu mateso yake na faraja yake kupitia Yesu Kristo. Timotheo yuko pamoja naye pia.

Maelezo ya jumla

Neno "ninyi" katika barua hii ina maanisha watu wa kanisa la Korintho na kwa wakristo wengine katika eneo hilo. Inawezekana Timotheo anaandika kwenye karatasi iliyotengenezwa kwa ngozi mameno anayoyasema Paulo.

Huyu Paulo

Lugha yako inaweza kuwa hasa njia ya kumtambulisha mwandishi wa barua. AT: "Mimi, Paulo, niliandika barua hii."

kaka

Katika Agano Jipya, mtume Paulo mara nyingi alitumia neno "kaka" kumaanisha kwa wakristo wenzangu, kwa kuwa waumini wote katika Kristo ni watu wa familia moja ya kiroho, na Mungu kama Baba yao wa mbinguni.

Akaya

Hili ni jina la jimbo la Kirumi kusini mwa sehemu iitwayo Ugiriki kwa sasa.

Neema iwe kwenu na amani

Neno "kwenu" ina maanisha watu wa kanisa la Koritho na kwa wakristo wengine katika eneo hilo. Hii nisalamu ya kawaida ya Paulo katika barua hizi.