sw_tn/luk/23/intro.md

1.2 KiB

Luka 23 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

ULB huweka mbele kidogo mstari wa mwisho wa sura hii kwa sababu unaunganishwa zaidi na sura ya 24 kuliko sura ya 23.

Dhana maalum katika sura hii

"Walianza kumshtaki"

Watu hawa hawakuwa wakimshtaki Yesu kwa kufanya uovu, bali mashtaka yao yalikuwa ya uwongo. Waligeuza ukweli ili kumfanya Pilato kumhukumu Yesu kufa.

"Pazia la hekalu likagawanyika na kuwa vipande viwili"

Hii ni ishara muhimu. Pazia ilikuwa mfano ya utenganisho kati ya Mungu na mwanadamu. Mungu hakuweza kupatikana moja kwa moja kwa sababu ya utakatifu wake. Kifo cha Kristo kilibadilisha hii. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/holy)

Desturi ya Mazishi

Ilikuwa ni desturi katika Israeli ya kale kumzika mtu aliyeheshimika katika kaburi na kutumia mwamba mkubwa kuifunga.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Sioni kosa lolote katika mtu huyu.""

Baada ya swali moja rahisi, inaonekana kwamba Pilato anamtangaza Yesu kutokuwa na hatia haraka sana. Hii ni kwa sababu Luka hajaweka maelezo mengi ya mazungumzo ya Yesu na Pilato. Habari hii imeandikwa katika Injili nyingine.

<< | >>