sw_tn/luk/24/intro.md

1.6 KiB

Luka 24 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Imani ya wanawake

Katika sura hii inaonekana kuwa Luka kwa makusudi anatofautisha imani ya wanawake na imani ya wanafunzi kumi na wawili.

Ufufuo

Luka katika sura hii anatumia maelezo mengi ili kuonyesha ufufuo wa Yesu kutoka kwa wafu. Luka anaonyesha kwamba haikuwezekana kwa mtu mwingine kufa kwa niaba ya Yesu. Anaonyesha pia kwamba ufufuo haukuwa mfano. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/resurrection]] and [[rc:///ta/man/translate/figs-metaphor]])

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Mwana wa Binadamu"

Yesu anajiita mwenyewe kama "Mwana wa Binadamu." Lugha zingine haziwezi kuruhusu mtu kujitaja mwenyewe kama 'mtu wa tatu.'

"Siku ya tatu"

Inasemekana kuwa Yesu alifufuka kutoka wafu siku ya tatu. Alikufa siku ya Ijumaa alasiri (kabla ya kutua kwa jua) na kufufuliwa Jumapili. Katika Israeli ya kale, siku ilianza na kumalizika wakati wa kutua kwa jua. Pia walihesabu sehemu yoyote ya siku kama "siku."

Watu wawili wenye mavazi ya kuangaza

Mathayo, Marko, Luka, na Yohana wote waliandika juu ya malaika waliovalia nguo nyeupe wakiwa pamoja na wanawake katika kaburi la Yesu. Waandishi wawili kati yao waliwaita wanaume, lakini ni kwa sababu tu malaika walikuwa katika hali ya kibinadamu. Waandishi wawili waliandika kuhusu malaika wawili, lakini waandishi wengine wawili waliandika juu ya moja tu. Ni bora kutafsiri kila moja ya vifungu hivi kama inavyoonekana katika ULB bila kujaribu kufanya vifungu vyote kufanana. (Angalia: Mathayo 28:1-2, Marko 16: 5 na Luka 24: 4 na Yohana 20:12)

__<< | __