sw_tn/luk/21/intro.md

1.3 KiB

Luka 21 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Luka 21:5-36 ni mafundisho yaliyopanuliwa kuhusu kurudi kwa Kristo.

Dhana maalum katika sura hii

"Kwa maana wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, 'Mimi ndiye,'"

Yesu anafundisha kwamba kabla ya kurudi kwake watu wengi watajidai kuwa ni yeye anayerudi. Pia itakuwa wakati wa mateso makubwa.

"Mpaka nyakati za Mataifa zitimizwe"

Wayahudi walizungumzia wakati kati ya uhamisho wa Babeli na kuja kwa Masihi kama kipindi cha utawala wa Wayunani. Hii ni kwa sababu Wayahudi hawakuwa na mamlaka juu ya mambo yao wenyewe.

Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii

Kusema kwa mifano

Unabii katika sura hii ina lugha ya kusema kwa mifano. Ni bora kutafsiri habari yalioandikwa kama matukio halisi isipokuwa tafsiri hii haiwezekani au inatoa maana isiyosawa. Kwa mfano, maneno "yamevunjwa," "yatasimama dhidi," na "hakuna nywele kichwani mwako itakayoangamia" ni mifano. "Ishara mbinguni," "tetemeko la ardhi," na "vita" lazima pia zitafsiriwe kwa uhalisi. (See: rc://*/ta/man/translate/figs-metaphor)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Mwana wa Binadamu"

Yesu anajiita mwenyewe kama "Mwana wa Binadamu." Lugha zingine haziwezi kuruhusu mtu kujitaja mwenyewe kama 'mtu wa tatu.'

<< | >>