sw_tn/luk/20/intro.md

1.4 KiB

Luka 20 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri hupendelea kuweka mbele kidogo nukuu za Agano la Kale. ULB na tafsiri nyingine nyingi za Kiingereza huingiza mistari ya 20:17, 42-43, ambayo ni nukuu kutoka Agano la Kale.

Dhana maalum katika sura hii

Mtego

Sura hii ina maswali mawili yaliyopangwa ili kumkamata mtu anayekubali kitu ambacho hataki kusema. Yesu anauliza swali kwa Mafarisayo ambalo linawatega kwa kuwalazimisha kukiri kwamba wanaamini Yohana Mbatizaji alikuwa nabii au kuwakasirisha Wayahudi kwa kukataa hili. Viongozi walijaribu kumtega Yesu kwa kumuuliza kuhusu kulipa kodi kwa serikali ya Kirumi. Kujibu ndiyo kungewakasirisha Wayahudi na kujibu hapana kungewakasirisha Warumi. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/prophet)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Kitendawili

Kitendawili ni taarifa inayoonekana kuwa ya ajabu, ambayo ni kana kwamba inajikana yenyewe, lakini sivyo. Katika sura hii, Yesu ananukuu Zaburi ambayo inasema Daudi anamwita mwanawe "bwana," yaani, "mkuu." Hata hivyo, kwa Wayahudi, mababu walikuwa wakubwa kuliko uzao wao. Katika kifungu hiki, Yesu anajaribu kuwaongoza wasikilizaji wake kuelewa kweli kwamba Masihi mwenyewe atakuwa Mungu, na kwamba yeye mwenyewe ndiye Masihi. (Luka 20:41-44).

<< | >>