sw_tn/deu/24/14.md

1.1 KiB

Taarifa ya Jumla:

Musa anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli kana kwamba walikuwa mtu mmoja, kwa hiyo maneno "yako" na "wako" hapa ni katika umoja.

Hautakiwi kumuonea mtumishi wa kuajiriwa

"Hautakiwi kumtendea mtumishi wa kuajiriwa vibaya"

mtumishi wa kuajiriwa

mtu ambaye hulipwa kila siku kwa kazi yake

maskini na muhitaji

Maneno haya mawili yana maana za kufanana na husisitiza ya kwamba mtu huyu hawezi kujisaidia mwenyewe.

ndani ya malango ya mji wako

Hapa "malango ya mji" ina maana ya miji au mjini. "moja ya miji yenu"

Kila siku unapaswa kumlipa mshahara wake

"Unapaswa kumpatia mwanamume pesa anayopata kila siku"

jua halipaswi kuzama kabla ya suala hili kutatuliwa

Hii ni lahaja. Waisraeli walichukulia siku mpya kuanza pale jua linapozama. "unatakiwa kumlipa mtu katika siku hiyo anayofanya kazi"

kwa maana ni maskini na anautegemea

Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "kwa sababu ni maskini na anategemea mshahara wake kununua chakula chake cha siku inayofuata"

asilie dhidi yako kwa Yahwe

"asipaze sauti kwa Yawhe na kumuomba akuadhibu"