# Taarifa ya Jumla: Musa anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli kana kwamba walikuwa mtu mmoja, kwa hiyo maneno "yako" na "wako" hapa ni katika umoja. # Hautakiwi kumuonea mtumishi wa kuajiriwa "Hautakiwi kumtendea mtumishi wa kuajiriwa vibaya" # mtumishi wa kuajiriwa mtu ambaye hulipwa kila siku kwa kazi yake # maskini na muhitaji Maneno haya mawili yana maana za kufanana na husisitiza ya kwamba mtu huyu hawezi kujisaidia mwenyewe. # ndani ya malango ya mji wako Hapa "malango ya mji" ina maana ya miji au mjini. "moja ya miji yenu" # Kila siku unapaswa kumlipa mshahara wake "Unapaswa kumpatia mwanamume pesa anayopata kila siku" # jua halipaswi kuzama kabla ya suala hili kutatuliwa Hii ni lahaja. Waisraeli walichukulia siku mpya kuanza pale jua linapozama. "unatakiwa kumlipa mtu katika siku hiyo anayofanya kazi" # kwa maana ni maskini na anautegemea Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "kwa sababu ni maskini na anategemea mshahara wake kununua chakula chake cha siku inayofuata" # asilie dhidi yako kwa Yahwe "asipaze sauti kwa Yawhe na kumuomba akuadhibu"