sw_tn/deu/24/14.md

37 lines
1.1 KiB
Markdown
Raw Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Taarifa ya Jumla:
Musa anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli kana kwamba walikuwa mtu mmoja, kwa hiyo maneno "yako" na "wako" hapa ni katika umoja.
# Hautakiwi kumuonea mtumishi wa kuajiriwa
"Hautakiwi kumtendea mtumishi wa kuajiriwa vibaya"
# mtumishi wa kuajiriwa
mtu ambaye hulipwa kila siku kwa kazi yake
# maskini na muhitaji
Maneno haya mawili yana maana za kufanana na husisitiza ya kwamba mtu huyu hawezi kujisaidia mwenyewe.
# ndani ya malango ya mji wako
Hapa "malango ya mji" ina maana ya miji au mjini. "moja ya miji yenu"
# Kila siku unapaswa kumlipa mshahara wake
"Unapaswa kumpatia mwanamume pesa anayopata kila siku"
# jua halipaswi kuzama kabla ya suala hili kutatuliwa
Hii ni lahaja. Waisraeli walichukulia siku mpya kuanza pale jua linapozama. "unatakiwa kumlipa mtu katika siku hiyo anayofanya kazi"
# kwa maana ni maskini na anautegemea
Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "kwa sababu ni maskini na anategemea mshahara wake kununua chakula chake cha siku inayofuata"
# asilie dhidi yako kwa Yahwe
"asipaze sauti kwa Yawhe na kumuomba akuadhibu"