sw_tn/act/07/intro.md

2.4 KiB

Matendo 07 Maelezo kwa Jumla

Muundo na Mpangilio

Tafsiri zingine zimeweka kila mstari wa ushairi mbele ya kulia kuliko maandishi mengine ili kurahisisha kusoma. ULB hufanya hivi na ushairi ambao umenukuliwa kutoka Agano la Kale 7:42-43 na 49-50.

Inaonekana kwamba 8:1 ni sehemu ya utungo wa sura hii.

Dhana maalum katika sura hii

"Stefano alisema"

Stefano alihadithia historia ya Israeli kwa ufupi. Alisisitiza ule muda Wana wa Israeli walikuwa wamewakataa watu Mungu alikuwa amechagua kuwaongoza. Mwisho wa habari, alisema viongozi wa Wayahudi aliokuwa akiwazungumzia walikuwa wamemkataa Yesu jinsi Waisraeli watenda dhambi walikuwa wakiwakataa viongozi walioteuliwa na Mungu.

"Jazwa na Roho Mtakatifu"

Roho Mtakatifu alimwongoza Stefano kana kwamba alisema tu kile Mungu alitaka aseme.

Kuashiria yajayo

Mwandishi anapolizungumzia jambo ambalo si muhimu kwa wakati huo lakini litakuja kuwa muhimu baadaye katoka hadithi hiyo, hii huitwa kuashiria yajayo. Luka anamtaja Saulo, aliyejulikana kama Paulo kwa hii hadithi ingawa si mhusika wa maana kwenye habari hii. Hii ni kwa maana Paulo ni mtu muhimu katika sehemu zilizobaki kwenye hiki kitabu cha Matendo ya Mitume.

Mifano muhimu za usemi katika Sura hii

Mawasiliano yaliyolengwa

Stefano alikuwa akizungumza na Wayahudi walizifahamu vyema sheria za Musa na kwa hivyo hakufafanua vitu ambavyo wasikilizaji wake walikuwa wanajua mbele. Lakini utahitajika kueleza baadhi ya vitu hivi ili wasomi wako waweze kuelewa alichokuwa anasema Stefano. Kwa mfano labda utaeleza vizuri kwamba wakati ndugu zake Yusufu "walimuuza Misri" (Matendo 7:9), Yosufu alikuwa anaenda kuwa mtumwa Misri, (tazama: rc://en/ta/man/translate/figs-metonymy)

Metonymy

Stefano alizungumzia Yusufu kuongoza "Juu ya Misri" na juu ya nyumba ya Farao. Hapa alimaanisha ya kwamba Yusufu aliongoza watu wa Misri na watu na mali yote iliyokuwa ndani ya nyumba ya Farao (Tazama: rc://en/ta/man/translate/figs-metonymy).

Matatizo mengine ya tafsiri katika sura hii

Maelezo ya awali

Viongozi wa Wayahudi ambao Stefano aliwazungumzuia walikuwa wanafahamu mbele matukio aliyokuwa akiwazungumzuia. Walifahamu kwamba Musa aliandika Kitabu cha Mwanzo. Kama kitabu cha mwanzo hakikutafsiriwa katika lugha yako, itakuwa vigumu kwa wasomaji wako kuelewa alichosema Stefano.

<< | >>