sw_tn/act/04/23.md

29 lines
814 B
Markdown

# Maelezo ya jumla
Wakinena pamoja, watu walinukuu Zaburi ya Daudi kutoka Agano la Kale.
# Maelezo ya jumla
Neno "wao" linamaanisha baadhi ya waumini, lakini si Petro na Yohana.
# Walikuja kwa watu wao
Walikwenda kwa waumini wenzao.
# kwa Roho Mtakatifu, kwa kinywa cha baba yetu Daudi, mtumishi wako, ulisema
Hii inamaanisha Roho Mtakatifu alisababisha Daudi kunena au kuandika kile Mungu alichosema.
# Kwa kinywa cha baba yetu Daudi
Neno "kinywa" linaelezea yale maneno ambayo Daudi aliyasema ama aliyaandika "Kwa maneno ya baba yetu Daudi"
# Kwanini watu wa mataifa wamefanya ghasia, na watu wametafakari mambo yasiyofaa?
Hili ni swali lenye jibu linaloelezea maneno yenye ubatili ya kumpinga Mungu.
# watu wametafakari mambo yasiyofaa
Watu wanatafakari maneno ya ubatili yaliyo kinyume na Mungu.