# Maelezo ya jumla Wakinena pamoja, watu walinukuu Zaburi ya Daudi kutoka Agano la Kale. # Maelezo ya jumla Neno "wao" linamaanisha baadhi ya waumini, lakini si Petro na Yohana. # Walikuja kwa watu wao Walikwenda kwa waumini wenzao. # kwa Roho Mtakatifu, kwa kinywa cha baba yetu Daudi, mtumishi wako, ulisema Hii inamaanisha Roho Mtakatifu alisababisha Daudi kunena au kuandika kile Mungu alichosema. # Kwa kinywa cha baba yetu Daudi Neno "kinywa" linaelezea yale maneno ambayo Daudi aliyasema ama aliyaandika "Kwa maneno ya baba yetu Daudi" # Kwanini watu wa mataifa wamefanya ghasia, na watu wametafakari mambo yasiyofaa? Hili ni swali lenye jibu linaloelezea maneno yenye ubatili ya kumpinga Mungu. # watu wametafakari mambo yasiyofaa Watu wanatafakari maneno ya ubatili yaliyo kinyume na Mungu.