sw_tn/2co/05/intro.md

1.7 KiB

2 Wakorintho 05 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Miili mipya mbinguni

Paulo anajua kwamba atakapokufa atapata mwili bora zaidi. Kwa sababu hii, yeye haogopi kuuawa kwa ajili ya kuhubiri injili. Kwa hiyo anawaambia wengine kwamba wao pia wanaweza kuunganishwa na Mungu. Kristo ataondoa dhambi zao na kuwapa haki yake. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/goodnews]], rc://en/tw/dict/bible/kt/reconcile and rc://en/tw/dict/bible/kt/sin and [[rc://en/tw/dict/bible/kt/righteous)

Uumbaji mpya

Uumbaji wa zamani na uumbaji mpya unaelezea jinsi Paulo anavyoonyesha Uumbaji wa zamani na uumbaji mpya. Dhana hizi pia ni sawa na mtu wa zamani na mtu mpya. Neno "zamani" labda halielezei asili ya dhambi ambayo mtu anazaliwa nayo. Inamaanisha njia ya zamani ya kuishi au Mkristo aliyekuwa amefungwa katika dhambi. "Uumbaji mpya" ni asili mpya au maisha mapya ambayo Mungu humpa mtu baada ya kumwamini Kristo. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/faith)

Mfano muhimu ya matamshi katika sura hii

Nyumbani

Nyumbani mwa Wakristo haipo tena ulimwenguni. Nyumbani halisi mwa Mkristo iko mbinguni. Kwa kutumia mfano huu, Paulo anasisitiza kuwa mazingira ya Kikristo katika ulimwengu huu ni ya muda mfupi. Inatoa tumaini kwa wale wanaosumbuliwa. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/heaven]] and rc://en/ta/man/translate/figs-metaphor and [[rc://en/tw/dict/bible/kt/hope)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Ujumbe wa upatanisho"

Hii inahusu injili. Paulo anawaita watu ambao wana chuki kwa Mungu kutubu na kuunganishwa naye. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/repent]] and [[rc://en/tw/dict/bible/kt/reconcile)

<< | >>