sw_tn/1th/04/intro.md

963 B

1 Wathesalonike 04 Maelezo kwa ujumla

Dhana muhimu katika sura hii

Uzinzi

Mila mbalimbali zina vipimo tofauti vya uzinzi na kwa hivyo itakuwa vigumu kutafsiri fungu hili.Watafsiri pia ni lazima wafahamu miiko ya kitamaduni. Maneno haya ni maneno yasiofaa kwa adabu sahihi.

Kufa kabla ya kurudi kwa Kristo

Katika kanisa la mwanzo, watu walijiuliza chenye kingefanyika iwapo mtu angekufa kabla ya kurudi kwake Yesu Kristo. Kuna uwezekano kwamba walikuwa na wasiwasi kama waliokufa kabla ya kurudi kwake Kristo wangejumuishwa kwenye ufalme wake. Paulo anajibu swali hilo.

"Kunyakuliwa mawinguni tumlaki Bwana hewani"

Kifungu hiki kinaashiria wakati Yesu atakapowaita wale waliomwamini. Wasomi wanatofautiana iwapo hii inaashiria kurudi kwake Yesu kwa mara ya mwisho kwa utukufu ama hapana. (Tazama:rc://en/tw/dict/bible/kt/believe)

<< | >>