sw_tn/1pe/02/intro.md

1.2 KiB

1 Petero 02 Maelezo kwa jumla

Muundo na mpangilio

Watafsiri wengine wametenga mistari ya ushairi mbele zaidi kuelekea kulia kuliko maandishi mengine ili yasomeke kwa urahisi. ULB hufanya hivi na ushairi ambao umenukuliwa kutoka Agano la kale katika 2:6, 7, 8 na 22.

Dhana muhimu katika sura hii

Mawe

Bibilia inatumia jengo lililojengwa kwa mawe makubwa kama mfano wa kanisa. Yesu ni jiwe kuu la pembeni, jiwe la muhimu. Mitume na manabii ndio msingi, sehemu ya jengo hili ambamo mawe mengine yanasimamia. Katika sura hii Wakristo ni mawe ambayo yanatengeneza kuta za jengo. (Tazama: rc://en/ta/man/translate/figs-metaphor and rc://en/tw/dict/bible/kt/cornerstone and rc://en/tw/dict/bible/other/foundation)

Mifano muhimu za usemi katika sura hii

Maziwa na watoto

Wakati Petero anawaambia wasomaji wake kwamba "watamani maziwa halisi ya kiroho", anatumia mfano ya mtoto mchanga ambaye hawezi kula chakula kigumu. Anataka kuwaelezea wasomaji wake kwamba wanaweza tu kuelewa vitu rahisi kuhusu maisha ya kumfurahisha Mungu. (Tazama: rc://en/ta/man/translate/figs-metaphor)

<< | >>