sw_tn/1pe/03/intro.md

1.1 KiB

1 Petero 03 Maelezo kwa jumla

Muundo na mpangilio

Watafsiri wengine wametenga mistari ya ushairi mbele zaidi kuelekea kulia kuliko maandishi mengine ili yasomeke kwa urahisi. ULB hufanya hivi na ushairi ambao umenukuliwa kutoka Agano la kale katika 3:10-12

Dhana muhimu katika sura hii

"Mapambo ya nje"

Watu wengi wanataka kuonekana wazuri ili watu wawapende na kufikiri ni watu wazuri. Wanawake huwa makini sana kuonekana wazuri kwa kuvalia nguo nzuri na mapambo. Petero anasema kwamba kile mtu anafikiri na kusema na kutenda ni muhimu kwa Mungu kuliko jinsi anavyoonekana.

Umoja

Petero alitaka wasomaji wake kukubaliana na kila mmoja wao. Muhimu zaidi aliwataka wapendane na kuvumiliana.

Mifano muhimu za usemi katika sura hii

Mfano

Petero ananukuu Zaburi ambayo inamfafanua Mungu kama mtu aliye na macho, masikio na uso. Hata hivyo Mungu ni roho na kwa hivyo hawezi kuwa na macho, masikio ama uso wa kibinadamu. Lakini yeye anafahamu wafanyacho watu na huwadhibu watu waovu. (Tazama: rc://en/ta/man/translate/figs-metaphor)

<< | >>