sw_tn/1jn/04/intro.md

946 B

1 Yohana 04 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Roho

Neno hili "roho" linatumiwa kwa njia tofauti katika sura hii. Wakati mwingine neno "roho" linamaanisha viumbe wa kiroho. Wakati mwingine inahusu tabia ya kitu fulani. Kwa mfano "roho ya mpinga Kristo," "roho ya kweli," na "roho ya hitilafu" inamaanisha kile ambacho ni mfano wa mpinga Kristo, ukweli, na kosa. "Roho" (iliyoandikwa na herufi kubwa "R") na "Roho wa Mungu" inamaanisha Mungu. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/antichrist)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Kupenda Mungu

Ikiwa watu wanampenda Mungu, wanapaswa kuonyesha katika njia wanayoishi na jinsi wanavyowatendea watu wengine. Kufanya hivyo kunaweza kutuhakikishia kuwa Mungu ametuokoa na kwamba sisi ni wake, lakini kupenda wengine haituokoi. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/save)

<< | >>