sw_tn/1jn/03/intro.md

1.2 KiB

1 Yohana 03 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Watoto wa Mungu

Mungu aliumba watu wote, lakini watu wanaweza tu kuwa watoto wa Mungu kwa kumwamini Yesu. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/believe)

Kaini

Kaini alikuwa mwana wa mtu wa kwanza, Adamu, na mwanamke wa kwanza, Hawa. Alimwonea wivu ndugu yake na kumwua. Wasomaji hawawezi kujua Kaini ni nani ikiwa hawajasoma kitabo cha Mwanzo. Wanaweza kusaidiwa ikiwa unawaelezea hivi.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Kujua"

Kujua" ni neno la kitenzi kinachotumika kwa njia mbili tofauti katika sura hii. Wakati mwingine hutumiwa kuhusu kujua ukweli, kama katika 3:2, 3:5, na 3:19. Wakati mwingine inamaanisha uzoefu na kuelewa mtu au kitu, kama katika 3:1, 3:6, 3:16, na 3:20. Lugha zingine zina maneno tofauti kwa maana hizi tofauti.

"Yeye anayezingatia amri za Mungu anakaa ndani yake, na Mungu anakaa ndani yake"

Wasomi wengi wanaamini kama hii inamaanisha kubaki katika mapenzi ya Mungu wala sio kumaanisha kuokolewa. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/eternity]] and [[rc://en/tw/dict/bible/kt/save)

<< | >>