sw_tn/1jn/02/intro.md

1.3 KiB

1 Yohana 02 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Mpinga Kristo

Katika sura hii Yohana anaandika juu ya mpinga Kristo maalum na wapinga Kristo wengi. Neno "mpinga Kristo" linamaanisha "anayepinga Kristo." Mpinga Kristo ni mtu atakayekuja siku za mwisho na kuiga kazi ya Yesu, lakini ataifanya kwa uovu. Kabla ya mtu huyu kuja, kutakuwa na watu wengi wanaofanya kazi dhidi ya Kristo; wao pia huitwa "wapinga Kristo." (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/antichrist]] and rc://en/tw/dict/bible/kt/lastday and [[rc://en/tw/dict/bible/kt/evil)

Mifano muhimu ya matamshi katika sura hii

Mfano

Kuna makundi kadhaa ya ya mifano yenye kufanana ambao yanatumiwa katika sura hii.

Kuwa ndani ya Mungu ni mfano ya kuwa na ushirika pamoja na Mungu, pia neno la Mungu na ukweli kuwa ndani ya watu ni mfano ya watu kujua na kutii neno la Mungu.

Kutembea ni mfano ya tabia, kutojua ambapo mtu anaenda ni mfano ya kutojua jinsi ya kuishi, na kujikwaa ni mfano ya dhambi.

Nuru ni mfano wa kujua na kufanya kile kilicho sahihi, na giza na upofu ni mfano ya kutojua kilicho sahihi na kutenda mabaya.

Watu wanaopotosha wengine ni mfano ya kufundisha watu mambo yasiyo ya kweli. (See: rc://en/ta/man/translate/figs-metaphor)

<< | >>