sw_tn/1co/08/intro.md

637 B

1 Wakorintho 08 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Katika Sura ya 8-10, Paulo anajibu swali hili: "Je, inakubalika kula nyama ambayo imetolewa dhabihu kwa sanamu?"

Dhana maalum katika sura hii

Nyama iliyotolewa dhabihu kwa sanamu

Paulo anajibu swali hili kwa kusema kwamba sanamu ni miungu ambayo haipo. Kwa hiyo hakuna ubaya wowote kwa hiyo nyama. Wakristo wana uhuru wa kula. Hata hivyo, mtu asiyeelewa hii anaweza kuona Mkristo akila. Wanaweza kisha kuhimizwa kula nyama kama kitendo cha ibada kwa sanamu.

<< | >>