sw_tn/1co/08/01.md

1.3 KiB

Sentensi Unganishi

Paulo anawakumbusha waumini kuwa ingawa sanamu hazina nguvu, waumini lazima wawe makini wasiwaathiri waumini dhaifu wanaoweza kufikiri wanatumikia sanamu. Paulo anawaambia waumini wawe makini katika uhuru walinao kwa Kristo.

Maelezo ya Jumla

"Sisi" inamaanisha Paulo pamoja na waumini wengine.

Sasa kuhusu

Paulo anatumia maneno haya kwenda kwenye sawali lijalo alilokuwa ameulizwa na Wakoritho.

vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu

Watu wa imani ya kipagani walitoa nafaka, samaki, ndege, au nyama, kwa miungu yao. Kuhani alitoa sehemu ya dhabihu ili kuichoma kwenye madhabahu.Paulo anazungumzia sehemu iliyo baki, ambayo ilipaswa kurudishwa kwa waabudu au kuuzwa katika soko.

Tunajua kuwa "wote tuna maarifa"

Paulo ananukuu maneno ambayo baadhi ya Wakoritho waliyatumia. "Wote tunajua, kama vile ninyi wenyewe mnapenda kusema, kwamba 'wote tuna maarifa.' "

Maarifa huleta majivuno

" Watu wenye ujuzi mwingi hufikiri wao ni bora zaidi kuliko hali yao halisi."

upendo hujenga

"Upendo ndiyo msaada wa kweli kwa watu"

mtu huyo anajulikana na yeye

"Mungu anamjua mtu huyo"

anadhani kwamba anajua jambo fulani

" anaamini anajua kila kitu kuhusu jambo fulani"

mtu huyo anajulikana naye

katika muundo tendaji "Mungu anamjua mtu huyo"