sw_tn/1co/03/intro.md

1.3 KiB

1 Wakorintho 03 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri huweka nukuu kutoka kwa Agano la Kale upande wa kulia zaidi kwenye ukurasa ili iwe rahisi kusoma. ULB inafanya hivyo kwa maneno yaliyotajwa kwenye mistari ya 19 na 20.

Dhana maalum katika sura hii

Watu wa kimwili

Waumini wa Korintho walikuwa hawajakomaa kwa sababu ya vitendo vyao vibaya. Anawaita "wa kimwili," maana matendo yao ni kama ya wasioamini. Neno hili linatumika kwa kinyume na wale ambao ni wa "kiroho." Wakristo wanaofuata "mwili" wao wanatenda upumbavu. Wao wanafuata hekima ya ulimwengu. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/righteous]], rc://en/tw/dict/bible/kt/flesh, rc://en/tw/dict/bible/kt/spirit and rc://en/tw/dict/bible/kt/foolish and [[rc://en/tw/dict/bible/kt/wise)

Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii

Mifano

Kuna mifano nyingi katika sura hii. Paulo anatumia "watoto" na "maziwa" ili kuonyesha kutokomaa kwa kiroho. Anatumia mifano nyingi na kumwagilia maji ili kuelezea majukumu yake na Apolo katika kukuza kanisa la Korintho. Paulo anatumia mifano mingine katika kusaidia kufundisha ukweli wa kiroho kwa Wakorintho na kuwasaidia kuelewa mafundisho yake. (See: rc://en/ta/man/translate/figs-metaphor)

<< | >>