sw_tn/1co/01/intro.md

1.9 KiB

1 Wakorintho 01 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Aya tatu za kwanza ni salamu. Katika inchi za kale za Mashariki ya Karibu, hii ilikuwa njia ya kawaida ya kuanzisha barua.

Baadhi ya tafsiri huweka kila mstari wa mashairi upande wa kulia zaidi kuliko maandiko yote ili iwe rahisi kusoma. ULB hufanya hivi kwa maneno ya mstari wa 19, ambayo yanayotoka Agano la Kale.

Dhana maalum katika sura hii

Mgongano

Katika sura hii, Paulo anakaripia kanisa kwa kugawanyika na kwa kufuata mitume tofauti. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/apostle)

Vipaji vya kiroho

Vipaji vya kiroho ni uwezo usio wa kawaida wa kusaidia kanisa. Roho Mtakatifu anatoa vipaji hivi kwa Wakristo baada ya kumwamini Yesu. Paulo anaorodhesha vipaji vya kiroho katika Sura ya 12. Wasomi wengine wanaamini kwamba Roho Mtakatifu alitoa baadhi ya vipaji hivi katika kanisa la kwanza tu ili kusaidia kuanzisha kanisa. Wasomi wengine wanaamini kwamba vipaji vyote vya Roho bado vinapatikana ili kuwasaidia Wakristo wote katika historia ya kanisa. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/faith)

Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii

Misemo

Katika sura hii, Paulo anaelezea kurudi kwa Kristo kwa kutumia maneno mawili tofauti: "ufunuo wa Bwana wetu Yesu Kristo" na "siku ya Bwana wetu Yesu Kristo." (See: rc://en/ta/man/translate/figs-idiom)

Maswali ya uhuishaji

Paulo hutumia maswali ya uhuishaji ili kuwakaripia Wakorintho kwa kugawanyika katika vikundi na kwa kutegemea hekima ya kibinadamu. (See: rc://en/ta/man/translate/figs-rquestion)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Kikwazo

Kikwazo ni mwamba ambamo watu wanajikwaa. Hapa ina maana kwamba Wayahudi wanaona vigumu kuamini kuwa Mungu alimruhusu Masihi wake kusulubiwa. (See: rc://en/ta/man/translate/figs-metaphor)

| >>