sw_tn/1co/front/intro.md

6.6 KiB

Utangulizi wa 1 Wakorintho

Sehemu ya 1: Utangulizi wa Ujumla

Maelezo ya Kitabu cha 1 Wakorintho

  1. Mgawanyiko katika kanisa (1:10-4:21)
  2. Dhambi na makosa (5:1-13)
  3. Wakristo kuwapeleka Wakristo wengine mahakamani (6:1-20)
  4. Ndoa na mambo yanayohusiana nayo (7:1-40)
  5. Uovu wa uhuru wa Kikristo; chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu, kukimbia ibada ya sanamu; kufunika kwa vichwa vya wanawake (8:1-13; 10:1-11:16)
  6. Haki za Paulo kama mtume (9:1-27)
  7. Meza ya Bwana (11:17-34)
  8. Vipaji vya Roho Mtakatifu (12:1-31)
  9. pendo (13:1-13)
  10. Vipaji vya Roho Mtakatifu: unabii na lugha (14:1-40)
  11. Ufufuo wa waumini na ufufuo wa Kristo (15:1-58)
  12. Kufunga: mchango wa Wakristo huko Yerusalemu, maombi, na salamu za kibinafsi (16:1-24)

Nani aliandika Kitabu cha 1 Wakorintho?

Paulo aliandika 1 Wakorintho. Paulo alitoka mji wa Tarso. Alikuwa anajulikana kama Sauli katika maisha yake ya awali. Kabla ya kuwa Mkristo, Paulo alikuwa Mfarisayo. Aliwatesa Wakristo. Baada ya kuwa Mkristo, alisafiri mara kadhaa katika Ufalme wa Roma akiwaambia watu kuhusu Yesu.

Paulo alianzisha kanisa lililokutana huko Korintho. Alikuwa akiishi katika mji wa Efeso wakati aliandika barua hii.

Je, kitabu cha 1 Wakorintho kinahusu nini?

1 Wakorintho ni barua ambayo Paulo aliwaandikia waumini waliokuwa katika mji wa Korintho. Paulo alikuwa amesikia kwamba kuna matatizo kati ya waumini huko. Walikuwa wakigombana. Baadhi yao hawakuelewa baadhi ya mafundisho ya Kikristo. Na baadhi yao walikuwa na tabia mbaya. Katika barua hii, Paulo aliwajibu na kuwahimiza kuishi kwa njia iliyopendeza Mungu.

Je, kichwa cha kitabu hiki kinapaswa kutafsiriwaje?

Watafsiri wanaweza kuchagua kuita kitabu hiki kwa kichwa chake cha jadi, "Wakorintho wa Kwanza." Au wanaweza kuchagua kichwa wazi, kama "Barua ya kwanza ya Paulo kwa Kanisa la Korintho." (See: rc://en/ta/man/translate/translate-names)

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za Kidini na za Kitamaduni

Mji wa Korintho ulikuwaje?

Korintho ilikuwa mji mkuu katika Ugiriki wa kale. Kwa sababu ulikuwa karibu na Bahari ya Mediterane, wasafiri wengi na wafanyabiashara walikuja kununua na kuuza bidhaa huko. Hii ilisababisha mji kuwa na watu kutoka tamaduni nyingi tofauti. Mji huo ulijulikana kwa kuwa na watu waliokuwa wameishi katika njia za uasherati. Watu waliabudu Afrodito, mungu wa kike wa Kigiriki wa upendo. Kama sehemu ya sherehe za kuheshimu Afrodito, waabudu wake walifanya ngono na makahaba wa hekalu.

Tatizo lilikuwa nini kwa nyama iliyotolewa kwa sanamu?

Wanyama wengi waliuawa na kutolewa dhabihu kwa miungu ya uongo huko Korintho. Wakuhani na waabudu walishika sehemu ya nyama hizo. Sehemu kubwa ya nyama hizo ilikuwa ikiuzwa katika masoko. Wakristo wengi hawakukubaliana iwapo ilikuwa ni sawa kula nyama hii, kwa sababu ilikuwa imetolewa kwa mungu wa uwongo. Paulo anaandika juu ya shida hii katika 1 Wakorintho.

Sehemu ya 3: Masuala muhimu ya Tafsiri

Je, mawazo ya "takatifu" na "kutakasa" yamewakilishwa vipi katika 1 Wakorintho kwenye ULB?

Maandiko hutumia maneno kama haya ili kuonyesha moja kati ya mawazo mbalimbali. Kwa sababu hii, mara nyingi ni vigumu kwa watafsiri kuyawakilisha vizuri katika tafsiri zao. Katika kutafsiri kwa Kiingereza, 1 Wakorintho kwenye ULB hutumia kanuni zifuatazo:

  • Wakati mwingine maana katika kifungu inaashiria utakatifu wa maadili. Hasa muhimu kuelewa katika injili kuwa ni ukweli kwamba Mungu anawaona Wakristo kuwa wasio na dhambi kwa sababu wameungana na Yesu Kristo. Ukweli mwingine unaohusiana na haya ni kwamba Mungu ni mkamilifu na hana hatia. Ukweli wa tatu ni kwamba Wakristo wanapaswa kujiendesha kwa njia isio na hatia na isiyo na hatia katika maisha. Katika hali hizi, ULB inatumia "takatifu," "Mungu mtakatifu," "watakatifu," au "watu watakatifu." (Angalia: 1:2; 3:17)
  • Wakati mwingine maana katika kifungu inaonyesha rejeo rahisi kwa Wakristo bila kuashiria jukumu fulani wanayopaswa kufanya. Katika nyakati hizi, ULB hutumia "mwamini" au "waumini." (Angalia: 6:1, 2, 14:33; 16:1,15)
  • Wakati mwingine maana katika kifungu hiki inaashiria mtu au kitu kilichowekewa Mungu peke yake. Katika matukio haya, ULB inatumia "kuwekwa kando," "kujitolea," "iliyohifadhiwa," au "kutakaswa." (Angalia: 1:2; 6:11; 7:14,34)

UDB mara nyingi husaidia ikiwa wafasiri wanafikiria juu ya jinsi ya kuwakilisha mawazo haya katika tafsiri zao wenyewe.

Nini maana ya "mwili"?

Paulo mara nyingi alitumia maneno "mwili" au "kimwili" kwa kutaja Wakristo ambao walifanya mambo ya dhambi. Hata hivyo, sio ulimwengu wa kimwili ambao ni mbaya. Paulo pia alielezea Wakristo ambao waliishi kwa njia ya haki kama "kiroho." Hii ni kwa sababu walifanya kile Roho Mtakatifu aliwafundisha kufanya. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/flesh]], rc://en/tw/dict/bible/kt/righteous and [[rc://en/tw/dict/bible/kt/spirit)

Paulo alimaanisha nini kwa maneno "katika Kristo," "katika Bwana," na kadhalika?

Maneno haya hutokea katika 1:2, 30, 31; 3:1; 4:10, 15, 17; 6:11, 19; 7:22; 9:1, 2; 11:11, 25; 12: 3, 9, 13, 18, 25; 14:16; 15:18, 19, 22, 31, 58; 16:19, 24. Paulo alijaribu kueleza wazo la muungano wa karibu kati ya Kristo na waumini. Wakati huo huo, mara nyingi alitaka kuelezea maana nyingine pia. Ona, kwa mfano, "wale ambao wamejitolea katika Kristo Yesu" (1:2), ambako Paulo alimaanisha hasa kwamba waumini Wakristo wamejitolea kwa Kristo.

Tafadhali angalia utangulizi wa Kitabu cha Warumi kwa maelezo zaidi juu ya maneno haya.

Je, ni masuala gani muhimu katika Kitabu cha 1 Wakorintho?

Kwa aya zifuatazo, matoleo ya kisasa ya Biblia yanatofautiana na matoleo ya zamani. Watafsiri wanashauriwa kufuata matoleo ya kisasa ya Biblia. Hata hivyo, ikiwa katika wilaya ya watafsiri kuna Biblia ambazo zinasomwa kulingana na matoleo ya kale ya Biblia, watafsiri wanaweza kufuata hayo. Ikiwa ni hivyo, mistari hii inapaswa kuwekwa ndani ya mabano ya mraba ([]) ili kuonyesha kwamba labda asili yao sio 1 Wakorintho.

  • "Basi, tukuzeni Mungu kwa miili yenu." Baadhi ya matoleo ya zamani husema "Kwa hiyo, tukuzeni Mungu kwa miili yenu na katika roho zenu, ambayo ni ya Mungu." (6:20)
  • "Nilifanya hivyo ingawa mimi sikuwa chini ya sheria." (9:20) Baadhi ya matoleo ya zamani hayana kifungu hiki.
  • "kwa ajili ya dhamiri - dhamiri ya mtu mwingine." Baadhi ya matoleo ya zamani husoma "kwa sababu ya dhamiri: kwa maana dunia na kila kitu kilicho ndani yake ni ya Bwana: dhamiri ya mtu mwingine." (10:28)
  • "na kwamba mimi hutoa mwili wangu kuchomwa moto." (13: 3) Baadhi ya matoleo ya zamani yanasema, "na kwamba ninatoa mwili wangu ili nipate kujivunia."
  • "Lakini kama mtu hajui jambo hili, asitambuliwe." (14:38) Baadhi ya matoleo ya zamani husema, "Lakini ikiwa kuna mtu yeyote asiyejua jambo hilo, basi asijue."

(See: rc://en/ta/man/jit/translate-textvariants)