sw_tn/1co/01/01.md

1.3 KiB

sentesi unganishi

Paulo na Sosthenes wanato salamu za kwa waumini wa kanisa la Korintho

Maelezo ya Jumla

Maneno kama vile "ninyi" and "yanu" yanahusiana na wale ambao paulo aliwaandikia na alitumia kiwakilisha cha wingi.

Paulo...kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho

Hii ilikuwa ni namna ya mwandishi wa barua kujitambulisha kwa wasomaji wake : " mimi, Paulo niliwaandikia barua hii ninyi munaomwamini Mungu mlioko Korintho"

Sosthene ndugu yetu

Hii inaonesha kuwa Paulo na Wakorintho wanamfahamu vema Sosthene:" Sosthene ndugu yetu ambaye mimi na ninyi tunamfahamu"

wale ambao wamewekwa wakfu katika Yesu Kristo

Neno "kuwekwa wakfu" linamaana ya watu ambao Mungu amewapa kibali cha kumtukuza yeye. " hii ni kwa wale ambao Yesu Kristo amaewatenga kwa ajili ya Mungu" au " watu ambao Mungu amaewachukua na kuwatenga kwa ajili yake mwenyewe kwa wanamwamini Yesu Kristo"

ambao wameitwa kuwa watu watakatifu

Hii inaweza kuelezewa kwa kitenzi tendaji: " ambao Mungu amewaita kuwa watu watakatifu" kuna maana mbili zinazokubalika. 1) " wale ambao Mungu amewatenga kwa ajili yake mwenyewe" 2) wale ambao Mungu amewaita kujitenga na dhambi" au ambao Mungu amewaita wajitenge na matendo ya dhambi"

Bwana wao na wetu

Yesu ni Bwana kwa Paul na kwa Wakorintho na ni Bwana kwa makanisa yote na watu wote