sw_tn/tit/01/10.md

802 B

sentensi unganishi

Kwa sababu ya wale wanaopinga neno la Mungu, Paulo anampa Tito sababu za kufundisha Neno la Mungu na kumwonya kuhusu waalimu wa uongo.

watu waasi

Hawa ni watu waasi waliokuwa wakiupinga ujumbe wa injili ya Paulo.

Wale wa tohara

inarejea wakristo wa Kiyahudi walikuwa wakifundisha kwamba ili kumfuata Kristo, mtu lazima atahiriwe.

Maneno yao ni upuuzi

'Maneno yao hayana faida yoyote"

Ni muhimu kuwakataza

"Ni lazima kuwazuia wasieneze mafundisho yao" au "Ni lazima kuwakataza kwa ushawishi wa maneno yao"

yale wasiyotakiwa kufundisha

Vitu ambavyo si sahihi kuvifundisha kuhusu Kristo na sheria.

Kwa faida ya aibu

"Hii inarejela faida ambayo watu wanapata kwa kufanya mambo yasiyo na heshima.

Wanaharibu nyumba nzima

"huharibu imani za familia yote"