# sentensi unganishi Kwa sababu ya wale wanaopinga neno la Mungu, Paulo anampa Tito sababu za kufundisha Neno la Mungu na kumwonya kuhusu waalimu wa uongo. # watu waasi Hawa ni watu waasi waliokuwa wakiupinga ujumbe wa injili ya Paulo. # Wale wa tohara inarejea wakristo wa Kiyahudi walikuwa wakifundisha kwamba ili kumfuata Kristo, mtu lazima atahiriwe. # Maneno yao ni upuuzi 'Maneno yao hayana faida yoyote" # Ni muhimu kuwakataza "Ni lazima kuwazuia wasieneze mafundisho yao" au "Ni lazima kuwakataza kwa ushawishi wa maneno yao" # yale wasiyotakiwa kufundisha Vitu ambavyo si sahihi kuvifundisha kuhusu Kristo na sheria. # Kwa faida ya aibu "Hii inarejela faida ambayo watu wanapata kwa kufanya mambo yasiyo na heshima. # Wanaharibu nyumba nzima "huharibu imani za familia yote"