sw_tn/rom/12/intro.md

1.4 KiB

Warumi 12 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri huweka kila mstari wa mashairi upande wa kulia zaidi kuliko maandiko yote ili iwe rahisi kusoma. ULB inafanya hivyo kwa maneno ya mstari wa 20, ambayo yanayotoka Agano la Kale.

Wasomi wengi wanaamini kwamba Paulo anatumia neno "kwa hiyo" katika Warumi 12:1 kurejea kwenye Sura zote za 1-11. Baada ya kuelezea kwa uangalifu injili ya Kikristo, Paulo sasa anaelezea jinsi Wakristo wanapaswa kuishi kulingana na ukweli huu mkubwa. Sura ya 12-16 inazingatia kuishi kwa imani ya Mkristo. Paulo anatumia amri nyingi tofauti katika sura hizi kutoa maelekezo haya ya vitendo. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/faith)

Dhana maalum katika sura hii

Kuishi Kikristo

Chini ya sheria ya Musa, watu walitakiwa kutoa dhabihu za hekalu za wanyama au nafaka. Sasa Wakristo wanatakiwa kuishi maisha yao kama aina ya dhabihu kwa Mungu. Dhabihu za kimwili hazihitajiki tena. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/lawofmoses)

Mifano muhimu ya matamshi katika sura hii

Mwili wa Kristo

Mwili wa Kristo ni sitiari muhimu au mfano inayotumiwa katika Maandiko kutaja kanisa. Kila mshiriki wa kanisa anafanya kazi ya kipekee na muhimu. Wakristo wanahitaji kila mmoja ya wenzao. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/body]] and [[rc:///ta/man/translate/figs-metaphor]])

<< | >>