sw_tn/rom/13/intro.md

1.4 KiB

Warumi 13 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Katika sehemu ya kwanza ya sura hii, Paulo anawafundisha Wakristo kutii viongozi wao. Wakati huo, watawala wa Kirumi wasiomcha Mungu walitawala nchi hiyo. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/godly)

Dhana maalum katika sura hii

Watawala wasiomcha Mungu

Wakati Paulo anafundisha juu ya kuitii watawala, wasomaji wengine wataona kuwa vigumu kuelewa, hasa katika maeneo ambapo watawala wanatesa kanisa. Wakristo lazima watii wakuu wao pamoja na kumtii Mungu, isipokuwa wakati watawala hawaruhusu Wakristo kufanya kitu ambacho Mungu anawaagiza. Kuna wakati ambapo mwamini lazima awe chini ya watawala hawa na kuteseka kwa mikono yao. Wakristo wanaelewa kwamba ulimwengu huu ni wa muda mfupi na watakuwa na Mungu milele. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/eternity)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Mwili

Hili ni suala gumu. Kuna uwezekano kuwa "Mwili" ni mfano ya asili yetu ya dhambi. Paulo hafundishi kwamba miili yetu ya kimwili ni dhambi. Inaonekana kuwa Paulo anafundisha kwamba wakati wote Wakristo wanaishi ("katika mwili"), tutaendelea kutenda dhambi. Lakini asili yetu mpya itapigana dhidi ya asili yetu ya zamani. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/flesh]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/sin]])

<< | >>