sw_tn/rom/12/01.md

1.4 KiB

Maelezo yanayounganisha:

Paulo anatuambia namna ambavyo maisha ya mwamini yanatakiwa yawe na namna waamini wanavyotakiwa kutumika.

Nawasihi Basi, ndugu, kwa huruma zake Mungu

"Waamini wenzangu, kwa sababu ya neemakuu ambayo Mungu ametupa nawasihi sana"

itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai

Hapa Paulo ametumia neno "miili" akimaanisha mtu. Paulo anamfananisha mwamini wa Kristo anayemtii Mungu na wanyama ambao Wayahudi waliwaua na kutoa sadaka kwa Mungu. "Mjitoe kabisa kwa Mungu mkiwa hai kama sadaka iliyokufa kwenye madhabahu hekaluni"

Takatifu, iliyokubalika na Mungu

Maana nyingine yaweza kuwa 1) "sadaka ambayo unampa Mungu pekee na itakayomtukuza" au 2) "Inayokubalika na Mungu kwa kuwa ni safi"

Hii ni huduma yenu ya kiroho

Inaweza kumaanisha 1) "Hii ni njia sahihi ya kumwabudu Mungu" au 2) "hii ndo namna ya kumwabudu Mungu kwenye roho zenu"

msiifuatishe namna ya dunia hii

Inamaanisha kwamba 1) "Msiishi kama dunia inavyoishi" au 2) Msifikirie kama dunia inavyofikiri."

Msiifuatishe

Hii inaweza kumaanisha 1) " Msiache dunia kuwaambia ni nini cha kufanya" au Msiache... nini cha kufikiria" au 2) "Msiruhusu kufanya kama dunia wanavyofanya"

Dunia hii

Hii inamaanisha watu wasioamini, wanaoishi katika dunia hii.

bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu.

"lakini muacheni Mungu awabadilishe namna mnavyofikiri" au "lakini mwacheni Mungu awabadilishe namna mnavyoenenda kwa kuwabadilisha kwanza namna mnavyofikiri"