sw_tn/rom/11/intro.md

1.5 KiB

Warumi 11 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri huweka kila mstari wa mashairi upande wa kulia zaidi kuliko maandiko yote ili iwe rahisi kusoma. ULB hufanya hivi kwa mistari 9-10, 26-27, na 34-35, ambayo ni maneno kutoka Agano la Kale.

Dhana maalum katika sura hii

Kupandikiza

Paulo anatumia mfano ya "kupandikiza" kutaja mahali pa Wayunani na Wayahudi katika mipango ya Mungu. Kufanya mmea mmoja kuwa sehemu ya kudumu ya mmea mwingine inaitwa "kupandikiza." Paulo anatumia taswira ya Mungu kupandikiza Wayunani kama tawi la mwitu katika mipango yake ya kuokoa. Lakini Mungu hajawasahau juu ya Wayahudi, ambao wanasemwa kuwa mmea wa asili. Mungu atawaokoa pia Wayahudi wanaomwamini Yesu.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Je, Mungu alikataa watu wake? Hata kidogo"

Ikiwa Waisraeli (wazao wa kimwili wa Abrahamu, Isaka na Yakobo) wako katika mipango ya Mungu ya baadaye, au ikiwa wamebadilishwa katika mipango ya Mungu na kanisa, ni suala kuu la kitheolojia katika Sura ya 9-11. Maneno haya ni ya muhimu katika sehemu hii ya Warumi. Inaonekana kuonyesha kwamba Israeli bado hutofautiana na kanisa. Si wasomi wote wanafikia hitimisho hili. Licha ya kwamba wao wanakataa Yesu sasa kama Masihi wao, Israeli haijapungukiwa na neema na huruma ya Mungu. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/christ]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/grace]] and rc://*/tw/dict/bible/kt/mercy)

<< | >>