sw_tn/rom/11/01.md

1.1 KiB

Maelezo yanayounganisha:

Japokuawa Israeli kama taifa lilikataliwa na Mungu, Mungu alitaka waelewe kuwa wokovu unakuja kwa neema bila kazi.

Basi naseema

"Mimi, Paulo, nikasema"

Je Mungu amewakataa watu wake?

Paulo alijiuliza hili swali ili awajibu maswali ya Wayahudi wengine waliokuwa wamekasirika kwamba Mataifa wamewekwa kuwa watu wa Mungu, wakati mioyo ya Wayahudi ikiwa imefanywa kuwa migumu.

Hata kidogo

"Hiyo haiwezekani" au "la hasha!" Ufafanuzi huu unakataa kwa nguvu kwamba hii haiwezi kutokea. Unaweza kuwa na ufafanuzi mwingine kwa lugha yako ambayo unaweza kutumia hapa.

Kabila la Benjamini

Hii inaelezea kabila ambalo ni kizazi cha Benjamini, moja kati ya makabila 12 ambayo Mungu aliwagawanya wana wa Israeli kwayo.

Aliowatambua

"Aliowafahamu tangu mwanzo"

Je, hamjui andiko linasema nini kuhusu Eliya, jinsi alivyomsihi Mungu juu ya Israeli?

"Hakika mnajua nini kimeandikwa kwenye maandiko. Mnakumbuka Eliya alivyomsihi Mungu juu ya Israeli."

Andiko linasema nini

Paulo anaelezea ni nini kimeandikwa kwenye maandiko.

Wao wamewauwa

"Wao" ni watu wa Israeli.

Nami nimesalia peke yangu

Neno "mimi" linamaanisha Eliya