sw_tn/rev/05/intro.md

1.4 KiB

Ufunuo 05 maelezo kwa jumla

Muundo na mpangilio

Tafsiri zingine zinaingiza ndani kidogo msitari wa ushairi ili isomeke kwa urahisi. ULB hufanya hivi na ushairi ulioko katika 4:8, 11

Dhana muhimu katika sura hii

Kitabo kilichofungwa na mihuri

Katika kitabu kilichofungwa na mihuri kimeandikwa ujumbe uliofichwa ambao unangojelewa kusomwa. Kitabu hiki kinaweza kusomwa tu na mtu aliye na mamlaka ya kukifungua.

Wazee ishirini na wanne

Labda maneno haya yanaashiria viongozi wa kanisa lakini utambulisho ya wazee ishirini na wanne sio na hakika. (Tazama: rc://*/ta/man/translate/writing-apocalypticwriting)

Sala za Kikristo

Sala za Wakristo zimeunganishwa na ubani. Sala za Wakristo zina harufu nzuri kwa Mungu. Mungu anafurahi wakati Wakristo wanapoomba.

Roho saba za Mungu

Maana halisi ya maneno haya haiko wazi. Kuna uwezekano kama ni mfano inayoashiria Roho Mtakatifu na nambari saba ikiashiria "ukamilifu." Kuna uwezekano kwamba pia si mfano, lakini inaashiria roho saba zinazozunguka kiti cha enzi cha Mungu.

Mifano muhimu ya usemi katika sura hii

Mfano

"Simba wa kabila la Yuda" na "mzizi wa Daudi" inaashiria Yesu. Hizi ni mifano inayotumika kama vyeo vya Yesu. (Tazama: [[rc:///ta/man/translate/figs-metaphor]] na [[rc:///ta/man/translate/figs-explicit]])

<< | >>