sw_tn/rev/02/intro.md

2.1 KiB

Ufunuo 02 Maelezo kwa Jumla

Muundo na mpangilio

Sura ya 2 na ya 3 pamoja zinaunda kitenge kimoja.Hii sehemu mara nyingi hujulikana kama "barua saba kwa makanisa saba."Mtafsiri anaweza amua kuzitenganisha barua hizi moja kwa nyingine ili kuzitofautisha.

Tafsiri zingine zinaingiza ndani kidogo nukuu kutoka Agano la kale. ULB hufanya hivi na nukuu kutoka 2:27

Dhana muhimu katika sura hii

Umaskini na Utajiri

Sura hii inatoa maana mbili ya kuwa maskini na kuwa tajiri.Waefeso walikuwa maskini wa kifedha kwa sababu hawakuwa na pesa nyingi. Hawakuwa maskini wa kiroho kwa sababu ya "utajiri mwingi" waliokuwa nao ndani ya Kristo. (Tazama: rc://*/tw/dict/bible/kt/spirit)

"Shetani ako karibu kufanya"

Kitabu cha Ufunuo kinahusu mambo ambayo Shetani atakuja kuyafanya duniani. Hata hivyo kinahusu kile ambacho Mungu atafanya mwishowe kumshinda Shetani.

Balaamu, Balaki na Jezebeli

Haya mafundisho juu ya Balaamu ni ngumu kuyaelewa iwapo vitabu vya Wafalme havijatafsiriwa. Kuna uwezekano kwamba hii inaashiria kuongoza watu wa Israeli kwa uzinzi na kwa kuabudu miungu wa uongo. (Tazama: rc://*/tw/dict/bible/kt/falsegod)

Tamathali muhimu za usemi katika sura hii

Mfano

Wasomi wengine wanachukulia sura ya 2 na 3 kama mfano. Wanaelewa kama makanisa haya ni aina ya makanisa ama vipindi vya kihistoria vya kanisa. Ni vema kutafsiri hii kama maelekezo ya makanisa ya kale katika miji hii. (Tazama: rc://*/ta/man/translate/figs-metaphor)

"Kama una sikio, sikia kile Roho anawaambia makanisa"

Maneno haya ni mwito wa kutubu kwa watu walio ndani ya kanisa. (Tazama: rc://*/tw/dict/bible/kt/repent)

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii

"Malaika wa makanisa saba"

Neno la Kigiriki "Malaika" linaweza pia kutafsiriwa kama "wajumbe."Kuna uwezekano hii inaashiria wajumbe ama viongozi wa makanisa haya saba.

"Haya ni maneno yake yule"

Haya maneno yanatumika kutanguliza barua hizi. Kuna uwezekano kama inaashiria Yesu. Kila barua basi inafafanua kipengele juu ya Yesu ambacho ni muhimu kwa barua nzima.

<< | >>