sw_tn/rev/01/intro.md

1.9 KiB

Ufunuo 01 Maelezo kwa jumla

Muundo na mpangilio

Sura hii inaelezea jinsi kitabu hiki ni kumbukumbu ya maono Yohana alipokea katika kisiwa cha Patmosi.

Tafsiri zingine zinaingiza ndani kidogo nukuu kutoka Agano la kale. ULB hufanya hivi na nukuu kutoka 1:7.

Dhana muhimu katika sura hii

Makanisa saba

Barua hii iliandikiwa makanisa saba halisi katika nchi inayotiwa sasa Uturuki.

Nyeupe

Rangi nyeupe huashiria utakatifu ama uadilifu katika maandiko. (Tazama: [[rc:///tw/dict/bible/kt/holy]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/righteous]])

Tamathali muhimu za usemi katika sura hii

"Yeye aliye, Aliyekuwepo, na atakayekuja"

Maneno haya yanaeleza kwamba Mungu amekuwepo, yupo sasa na atakuwepo milele. Siyo lugha zote zina njia ya kutafsiri kwa urahisi kipindi kilichopita, kipindi cha sasa na kipindi kijacho kwa kitenzi.Inaonekana huu ni mnyambuliko wa jina la Mungu, Yahweh, lenye maana "Mimi niko".

Damu yake

Hii inaashiria kifo cha Yesu. (Tazama: rc://*/ta/man/translate/figs-metonymy)

Maswala mengine ya utata katika tafsiri ya sura hii.

"Anakuja na mawingu"

Wasomi wengi wanaamini kwamba Yesu atarudi kwa awamu mbili. Kurudi kwa kwanza kwa Yesu kutakua wa kisiri kama "Mwizi wa usiku." Halafu Mungu atakuja kwa njia ya uwazi ambapo kila mtu atamuona. Huu ndio ujio wa mwisho uzungumzao kitabu cha Ufunuo.

Yesu

Taswira ya yule mwanaume aliye mbinguni ni ya Yesu. Kwa mtazamo wa jumla, taswira hii ni maelezo kuhusu Yesu katika utukufu yake. (Tazama: [[rc:///tw/dict/bible/kt/glory]] na [[rc:///ta/man/translate/figs-explicit]])

"Malaika wa makanisa saba"

Neno la Kigiriki linalotafsiriwa kama "malaika" linaweza kutafsiriwa pia kama "wajumbe." Kuna uwezekano hii inaashiria wajumbe ama viongozi wa makanisa haya saba.

| >>