Sura ya 2 na ya 3 pamoja zinaunda kitenge kimoja.Hii sehemu mara nyingi hujulikana kama "barua saba kwa makanisa saba."Mtafsiri anaweza amua kuzitenganisha barua hizi moja kwa nyingine ili kuzitofautisha.
Tafsiri zingine zinaingiza ndani kidogo nukuu kutoka Agano la kale. ULB hufanya hivi na nukuu kutoka 2:27
Sura hii inatoa maana mbili ya kuwa maskini na kuwa tajiri.Waefeso walikuwa maskini wa kifedha kwa sababu hawakuwa na pesa nyingi. Hawakuwa maskini wa kiroho kwa sababu ya "utajiri mwingi" waliokuwa nao ndani ya Kristo. (Tazama: [[rc://*/tw/dict/bible/kt/spirit]])
Haya mafundisho juu ya Balaamu ni ngumu kuyaelewa iwapo vitabu vya Wafalme havijatafsiriwa. Kuna uwezekano kwamba hii inaashiria kuongoza watu wa Israeli kwa uzinzi na kwa kuabudu miungu wa uongo. (Tazama: [[rc://*/tw/dict/bible/kt/falsegod]])
Wasomi wengine wanachukulia sura ya 2 na 3 kama mfano. Wanaelewa kama makanisa haya ni aina ya makanisa ama vipindi vya kihistoria vya kanisa. Ni vema kutafsiri hii kama maelekezo ya makanisa ya kale katika miji hii. (Tazama: [[rc://*/ta/man/translate/figs-metaphor]])
Haya maneno yanatumika kutanguliza barua hizi. Kuna uwezekano kama inaashiria Yesu. Kila barua basi inafafanua kipengele juu ya Yesu ambacho ni muhimu kwa barua nzima.