sw_tn/psa/109/028.md

24 lines
762 B
Markdown

# Ingawa wananilaani
Wanaozungumziwa ni watu wanaomshtaki Daudi na kusema vitu vibaya kumhusu.
# na waaibishwe
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "na waaibike" au "acha waaibike"
# lakini watumishi wako wafurahi
"lakini mimi, mtumishi wako, nifurahi" au "mimi ni mtumishi wako, acha nifurahi." Daudi anatumia msemo "mtumishi wako" kumaanisha ni yeye.
# Na washindani wangu wavikwe ... na wavae
Misemo hii miwili ina maana ya kufanana na inatumika kusisitiza jinsi anavyotamani sana waaibishwe.
# wavikwe aibu
Hapa Daudi anawazungumzia kuaibika kana kwamba ilikuwa vazi walilovaa. "waaibike sana"
# na wavae aibu yao kama joho
Daudi anawazungumzia kuaibika kana kwamba ilikuwa joho walilovaa. "na aibu yao iwafunike kama joho walilojifunika"