# Ingawa wananilaani Wanaozungumziwa ni watu wanaomshtaki Daudi na kusema vitu vibaya kumhusu. # na waaibishwe Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "na waaibike" au "acha waaibike" # lakini watumishi wako wafurahi "lakini mimi, mtumishi wako, nifurahi" au "mimi ni mtumishi wako, acha nifurahi." Daudi anatumia msemo "mtumishi wako" kumaanisha ni yeye. # Na washindani wangu wavikwe ... na wavae Misemo hii miwili ina maana ya kufanana na inatumika kusisitiza jinsi anavyotamani sana waaibishwe. # wavikwe aibu Hapa Daudi anawazungumzia kuaibika kana kwamba ilikuwa vazi walilovaa. "waaibike sana" # na wavae aibu yao kama joho Daudi anawazungumzia kuaibika kana kwamba ilikuwa joho walilovaa. "na aibu yao iwafunike kama joho walilojifunika"