sw_tn/mat/26/intro.md

2.1 KiB

Mathayo 26 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri zinaingiza nukuu kutoka kwa Agano la Kale. ULB inafanya hivyo kwa mistari iliyonukuliwa katika 26:31.

Dhana maalum katika sura hii

Kondoo

Hii ni taswira ya kawaida inayotumiwa katika Maandiko ya kutaja watu wa Israeli. Lakini, katika Mathayo 26:31, "kondoo" inawakilisha wanafunzi wa Yesu, ambao walikimbia wakati alikamatwa.

Pasaka

Kifo cha Yesu kilitokea kwa uhusiano na Sikukuu ya Pasaka kwa sababu yeye ndiye timizo la mwanakondoo wa Pasika. Ni kifo chake cha dhabihu ambacho kinatuokoa kutokana na hukumu ya Mungu.

Kula mwili na damu

Sherehe hii, ambayo mara nyingi huitwa "Meza ya Bwana," "Ekaristi", au "Ushirika Mtakatifu," hufanyika katika karibu makanisa yote hadi siku hii kwa ukumbusho wa dhabihu ya Kristo kwa ajili ya dhambi za binadamu. Hufanyika kwa kutii maagizo ya Yesu kwa wanafunzi wake katika Mathayo 26:26-28.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Aibu na woga

Kote katika sura hii, matendo ya viongozi wa Kiyahudi ni ya aibu na ya woga. Waliwaogopa watu waliopaswa kuwaongoza. Matendo yao ya aibu na ya uoga yanaweza kuwa vigumu kueleza katika kutafsiri.

Yuda kumbusu Yesu

Yuda amenakiliwa katika Mathayo 26:49 kumbusu Yesu ili kutoa ishara kwa askari ili kumtambua yule watakaomkamata. Miongoni mwa Wayahudi, kubusu ilikuwa njia ya kawaida ya kumsalimu mtu. Walikuwa na busu za aina mbalimbali kati ya watu wa tabaka mbalimbali. Kwa kuwa Yesu alikuwa mwalimu wa Yuda, labda alibusu mkono wake kama ishara ya heshima na utii.

"Haribu hekalu la Mungu"

Katika Mathayo 26:61, watu wawili wanamshtaki Yesu kwa kutaka hekalu la Yerusalemu liangamizwe ili aweze kulijenga kwa "siku tatu." Labda walikuwa wakimshtaki Yesu kwa kutukana hekalu na kwa hiyo, kwa njia nyingine, kumtukana Mungu. Mathayo hana rekodi ya Yesu akitamka haya, lakini maneno haya yapo katika Yohana 2:19.

Maneno "katika siku tatu" yanapaswa kueleweka kwa njia ya Kiyahudi kama "ndani ya siku tatu," wala sio "baada ya siku tatu."

<< | >>