sw_tn/mat/27/intro.md

1.6 KiB

Mathayo 27 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

"Walimpeleka kwa gavana Pilato"

Wayahudi walikuwa chini ya utawala wa Ufalme wa Kirumi, na Warumi hawakuwaruhusu watoe uhai wa mhalifu yeyote bila kupata ruhusa kwanza. Kwa hivyo viongozi wa Kiyahudi walimuomba Pontio Pilato athibitishe hukumu yao juu ya Yesu. Pilato alijaribu kuepuka kuthibitisha uamuzi wao. Alijaribu kuwafanya viongozi wa Kiyahudi kuchagua kati ya kumkomboa Yesu au mfungwa mbaya sana aliyeitwa Baraba.

Kaburi

Kaburi ambamo Yesu alizikwa (tazama: Mathayo 27:59-60) ilikuwa ni aina ya kaburi ambamo Wayahudi tajiri walizikwa. Ilikuwa na chumba halisi ambacho kilichombwa kwenye mwamba, ambapo miili ilikuwa imefungwa na kuwekwa kwenye miamba ilivyokuwa kwenye kuta. Baadaye, wakati miili imeharibika na kubakia mifupa iliyo wazi, mifupa hiyo ilikusanywa na kuingizwa kwenye mitungi maalum inayoitwa mabasi. Makaburi hayo yalifungwa na mwamba mmoja mkubwa wa kutosha kuufunga mlango. Mwamba huu ulikuwa umevingirwa au kuwekwa mahali pa mlango mwa kaburi.

Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii

"Shikamoo, Mfalme wa Wayahudi!"

Kifungu hiki, kinachopatikana katika Mathayo 27:29, ni mfano wa kinaya. Katika takwimu hii ya matamshi, kitu kinasemwa ili kuashiria kitu kingine, mara nyingi maana yake ikiwa ni kinyume. Tamko "Shikamoo" ilikuwa salamu iliyotumiwa na watu nyakati maalum, mara nyingi mbele ya wafalme na malkia. Hata hivyo, askari waliomdhihaki Yesu hawakutaka kumheshimu. (Angalia: rc://*/ta/man/translate/figs-irony)

<< | >>