sw_tn/mat/09/12.md

40 lines
1.1 KiB
Markdown

# Maelezo y a jumla
Matukio haya yanatokea kwenye nyumba ya Mathayo mtoza ushuru.
# Na Yesu aliposikia hayo
Hapa "hayo" inarejea swali ambalo mafarisayo waliuliza kuhusu Yesu kula na watoza ushuru na wenye dhambi.
# Watu walio na afya nzuri hawahitaji mganga, isipokuwa wale walio wagonjwa
Yesu anajibu kwa kutumia mithali. Anamaanisha kuwa anakula na watu wa aina hii kwa sababu amekuja kuwaokoa wenye dhambi.
# watu walio na afy nzuri
"watu wenye afya"
# wale walio wagonjwa
Kirai "wanahitaji mganga" kinaeleweka. "Wagonjwa ndio wanaohitaji mganga"
# Inawapasa muende mukajifunze maana yake
Yesu anaelekea kunukuu maandiko. "Inakupasa ujifunze maana ya kile ambacho Mungu alisema katika maandiko"
# Inawapasa muende
Kiwakilishi "wa" ni cha wingi kinachomaanisha mafarisayo
# Ninapenda rehema na wala siyo dhabihu
Yesu ananukuu kile ambacho nabii Hosea aliandika katika maandiko.. Hapa "Ni" inamaanisha Mungu.
# Kwa kuwa nilikuja
Hapa "Ni" inamaanisha Yesu.
# haki
Yesu anatumia kejeli. Hadhani kuwa kuna watu wenye haki ambao hawahitaji kutubu. "wale wanaodhani kuwa ni wenye haki"