# Maelezo y a jumla Matukio haya yanatokea kwenye nyumba ya Mathayo mtoza ushuru. # Na Yesu aliposikia hayo Hapa "hayo" inarejea swali ambalo mafarisayo waliuliza kuhusu Yesu kula na watoza ushuru na wenye dhambi. # Watu walio na afya nzuri hawahitaji mganga, isipokuwa wale walio wagonjwa Yesu anajibu kwa kutumia mithali. Anamaanisha kuwa anakula na watu wa aina hii kwa sababu amekuja kuwaokoa wenye dhambi. # watu walio na afy nzuri "watu wenye afya" # wale walio wagonjwa Kirai "wanahitaji mganga" kinaeleweka. "Wagonjwa ndio wanaohitaji mganga" # Inawapasa muende mukajifunze maana yake Yesu anaelekea kunukuu maandiko. "Inakupasa ujifunze maana ya kile ambacho Mungu alisema katika maandiko" # Inawapasa muende Kiwakilishi "wa" ni cha wingi kinachomaanisha mafarisayo # Ninapenda rehema na wala siyo dhabihu Yesu ananukuu kile ambacho nabii Hosea aliandika katika maandiko.. Hapa "Ni" inamaanisha Mungu. # Kwa kuwa nilikuja Hapa "Ni" inamaanisha Yesu. # haki Yesu anatumia kejeli. Hadhani kuwa kuna watu wenye haki ambao hawahitaji kutubu. "wale wanaodhani kuwa ni wenye haki"