sw_tn/luk/22/47.md

689 B

tazama, kundi kubwa la watu likatokea

Neno "tazama" linatutazamisha kuhusu kundi jipya katika simulizi.

akiwaongoza

Yuda alikuwa akiwaonyesha watu Yesu alipo. Alikuwa hawaambii kundi la watu nini cha kufanya. Tafsiri mbadala: "akiwaongoza kwa Yesu."

ili ambusu

"kumsalimia kwa busu" au "kumsalimia kwa kumbusu." Wakati wanaume walipowasalimia wanaume wengine ambao walikuwa wa familia au marafiki, waliwakumbatia.

je unamsaliti Mwana wa Adamu kwa busu

Yesu anatumia swali kumkemea Yuda kwa kumsaliti kwa busu. Kwa kawaida busu ni ishara ya upendo. Tafsiri mbadala: "Ni busu unayotumia kumsaliti Mwana wa Adamu!"

Mwana wa Adamu

Yesu anatumia neno hili kujiongelea yeye.