# tazama, kundi kubwa la watu likatokea Neno "tazama" linatutazamisha kuhusu kundi jipya katika simulizi. # akiwaongoza Yuda alikuwa akiwaonyesha watu Yesu alipo. Alikuwa hawaambii kundi la watu nini cha kufanya. Tafsiri mbadala: "akiwaongoza kwa Yesu." # ili ambusu "kumsalimia kwa busu" au "kumsalimia kwa kumbusu." Wakati wanaume walipowasalimia wanaume wengine ambao walikuwa wa familia au marafiki, waliwakumbatia. # je unamsaliti Mwana wa Adamu kwa busu Yesu anatumia swali kumkemea Yuda kwa kumsaliti kwa busu. Kwa kawaida busu ni ishara ya upendo. Tafsiri mbadala: "Ni busu unayotumia kumsaliti Mwana wa Adamu!" # Mwana wa Adamu Yesu anatumia neno hili kujiongelea yeye.