sw_tn/luk/10/05.md

1000 B

Amani iwe katika nyumba hii

Hii ilikuwa ni salamu na baraka. Hapa "nyumba" inawakilisha watu wanaoishi ndani ya nyumba. AT: "watu wa nyumba hii na wapokee amani."

mtu wa amani

"mtu mwenye amani." Huyu ni mtu anaetaka kuwa na amani na Mungu na watu.

amani yenu itabaki juu yake

AT: "atakuwa na amani aliyombarikia"

kama sivyo

AT: "kama hakuna mtu mwenye amani huko" au "mwenye nyumba sio mtu wa amani"

itarudi kwenu

"hatokuwa na hiyo amani" au "hatoipokea hiyo amani uliyombarikia"

Mbakie katika nyumba ile ile.

Yesu hakumaanisha waendelee kubakia ndani ya nyumba kwa siku nzima, ila wapate kulala katika nyumba mojakila usiku. AT:" Kuendelea kulala katika nyumba"

Mfanya kazi anasitahili mshahara wake

Yesu alikuwa alikuwa akizungumzia wale watu aliowatuma huko nje. Kwa sababu wangekuwa wakiwafundisha na kuwaponya watu, hivyo watu wangewapatia mahali pa kukaa pamoja na chakula.

Msiende nyumba kwa nyumba

AT:" Msilale sehemu/nyumba tofauti tofauti katika kila usiku"