# Amani iwe katika nyumba hii Hii ilikuwa ni salamu na baraka. Hapa "nyumba" inawakilisha watu wanaoishi ndani ya nyumba. AT: "watu wa nyumba hii na wapokee amani." # mtu wa amani "mtu mwenye amani." Huyu ni mtu anaetaka kuwa na amani na Mungu na watu. # amani yenu itabaki juu yake AT: "atakuwa na amani aliyombarikia" # kama sivyo AT: "kama hakuna mtu mwenye amani huko" au "mwenye nyumba sio mtu wa amani" # itarudi kwenu "hatokuwa na hiyo amani" au "hatoipokea hiyo amani uliyombarikia" # Mbakie katika nyumba ile ile. Yesu hakumaanisha waendelee kubakia ndani ya nyumba kwa siku nzima, ila wapate kulala katika nyumba mojakila usiku. AT:" Kuendelea kulala katika nyumba" # Mfanya kazi anasitahili mshahara wake Yesu alikuwa alikuwa akizungumzia wale watu aliowatuma huko nje. Kwa sababu wangekuwa wakiwafundisha na kuwaponya watu, hivyo watu wangewapatia mahali pa kukaa pamoja na chakula. # Msiende nyumba kwa nyumba AT:" Msilale sehemu/nyumba tofauti tofauti katika kila usiku"