sw_tn/luk/06/intro.md

2.5 KiB

Luka 06 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Luka 6:20-49 ina baraka na ole nyingi ambazo zinaonekana kuwa sawa na Mathayo 5-7. Sehemu hii ya Mathayo kwa kawaida inaitwa "Mahubiri ya Mlimani." Katika Luka, hayashikamani na mafundisho juu ya ufalme wa Mungu kama katika injili ya Mathayo. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/kingdomofgod)

Dhana maalum katika sura hii

"Kula nafaka"

Ilikuwa nazoezi yaliokubaliwa kwa wasafiri kuchuma na kula kiasi kidogo cha nafaka kutoka kwa mimea katika mashamba waliyoyapitia. Sheria ya Musa ililazimisha walimaji waruhusu wasafiri hivyoo. Wafarisay waliwaza kama kuchuma nafaka ni kazi ya "kukusanya masuke yaiyobaki" na sheria ya Musa inazuia kufanya kazi kwa siku ya Sabato. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/lawofmoses]], [[rc:///tw/dict/bible/kt/works]] and rc://*/tw/dict/bible/kt/sabbath)

Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii

Maneno yanayoonyesha mfano

Ilikuwa kawaida kwa Yesu kutumia maneno ya mifano kwa kufundisha watu ukweli usiyo rahisi wa kiroho. (See: rc://*/ta/man/translate/figs-metaphor)

Maswali ya uhuishaji

Yesu alitumia maswali ya uhuishaji ili kuwafundisha watu na kuwahukumu. (See: rc://*/ta/man/translate/figs-rquestion)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Maelezo yaliyodokezwa

Mara nyingi Luka anaandika habari yaliyoelewa kabisa na watu wa kale wa inchi za Mashariki ya Karibu lakini labda watu wa leo wa mazoezi tofauti hawaelewi. kwa mfano watu wanatarajia siku ya hukumu ya mwisho au labda hukumu kwa siku ya mwisho ya maisha yao (Luka 6:37). (See: rc://*/ta/man/translate/figs-explicit)

Wanafunzi kumi na wawili

Yafuatayo ni orodha ya wanafunzi kumi na wawili: Katika Mathayo: Simoni (Petro), Andrea, Yakobo mwana wa Zebedayo, Yohana mwana wa Zebedayo, Filipo, Bartholomayo, Tomasi, Mathayo, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni mzeloti na Yuda Iskarioti.

Katika Marko: Simoni (Petro), Andrea, Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana mwana wa Zebedayo (ambaye aliwaita Boanerge, yaani, wana wangurumo), Filipo, Bartholomayo, Mathayo, Tomasi, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni mzeloti, na Yuda Isikarioti.

Katika Luka: Simoni (Petro), Andrea, Yakobo, Yohana, Filipo, Bartholomayo, Mathayo, Tomasi, Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni (aitwaye mzeloti, Yuda mwana wa Yakobo, na Yuda Isikarioti.

Inawezekana kuwa Thadayo na Yuda, mwana wa Yakobo, ni majina mawili ya mtu mmoja.

<< | >>