sw_tn/luk/07/intro.md

1.9 KiB

Luka 07 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri hupendelea kuweka mbele kidogo nukuu za Agano la Kale. ULB na tafsiri nyingine nyingi za Kiingereza huingiza mistari yote ya 7:27, ambayo ni nukuu kutoka Agano la Kale.

Kuna nyakati katika maelezo ya sura hii ambapo kuna mabadiliko ya ghafla katika mada. Mtafsiri hapaswi kulainisha mabadiliko haya.

Dhana maalum katika sura hii

Jemadari

Hali hii haikuwa jambo la kawaida sana katika Israeli ya kale. Haikuwa kawaida kwa askari wa Kirumi kuhitaji chochote kwa Waisraeli kwani hawakuwa wa maana kwa Warumi na hawangehitaji uponyaji kutoka kwa Myahudi. Haikuwa pia kawaida kwa tajiri kujali maslahi ya mtumwa wake. Hii inaonyesha imani kuu. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/faith)

Ubatizo wa Yohana

Ubatizo ambao Yohana alifanya ulikuwa tofauti na ubatizo ambao kanisa linafanya. Ubatizo wa Yohana ulikuwa unaashiria kuwa wale waliopokea walikuwa wametubu dhambi zao. Ndio maana Mafarisayo hawakuhusika katika ubatizo wa Yohana. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/repent]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/sin]]).

"Wenye dhambi"

Luka anaashiria kundi la watu kuwa "wenye dhambi." Viongozi wa Kiyahudi waliona watu hawa kuwa hawaelewi Sheria ya Musa, na hivyo wakawaita "wenye dhambi." Kwa kweli, viongozi wenyewe ndio walikuwa wenye dhambi. Hali hii inaweza kuchukuliwa kama kinaya. (See: rc://*/ta/man/translate/figs-irony)

"Miguu"

Miguu ilionekana kuwa ni chafu sana katika inchi za Mashariki ya Karibu ya Kale. Ingekuwa tendo la unyenyekevu sana kwa mwanamke huyu kuosha miguu ya Yesu na ilikuwa njia ya kumheshimu Yesu.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Mwana wa Binadamu"

Yesu anajiita mwenyewe kama "Mwana wa Binadamu." Lugha zingine haziwezi kuruhusu mtu kujitaja mwenyewe kama 'mtu wa tatu.' (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/sonofman)

<< | >>