sw_tn/luk/05/intro.md

3.0 KiB

Luka 05 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

"Utavua watu"

Agano Jipya mara nyingi huzungumzia juu ya kufanya wanafunzi au wafuasi wa Kristo. Hii ni huduma kuu ya kanisa. Kuna takwimu nyingi tofauti zinazotumiwa kuelezea hii katika Agano Jipya. Katika sura hii, Yesu anatumia mfano wa uvuvi kueleza kuwa wanafunzi wa Kristo wanapaswa kukusanyika watu wengine wawe wanafunzi wa Kristo. Yesu anamsaidia mvuvi Simoni kuvua samaki wengi sana ili kuonyesha kwamba Yesu atawawezesha Simoni na wanafunzi wengine kukusanyika wau wengi kumfuata Kristo. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/disciple]] and [[rc:///ta/man/translate/figs-metaphor]])

"Watu wenye dhambi"

Mafarisayo hutaja kundi la watu kuwa "wenye dhambi." Walikuwa wanamaanisha ni watu ambao hawakuwa na nia ya kufuata Sheria ya Musa. Hata hivyo, Luka anatumia neno "wenye dhambi" kama maneno ya kuzihaka, kwa sababu Yesu anasema kwamba alikuja kuwaita wenye dhambi kutubu. Kwa kutaja "wenye dhambi," Yesu alikuwa akimaanisha mtu yeyote mwenye hatia ya dhambi. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/sin]] and [[rc:///ta/man/translate/figs-irony]])

Kufunga na Karamu

Kufunga mara nyingi kulifanyika wakati wa toba. Hakukufanyika wakati wa furaha. Kwa kuwa wakati ambapo Yesu alikuwa pamoja na wanafunzi wake ilikuwa wakati wa furaha, aliwaambia kama watafunga kwa wakati hayuko pamoja na wao tena. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/repent)

Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii

Hali ya Kufikiri

Yesu anatumia hali ya kufikiri kuwahukumu Mafarisayo. Kifungu hiki kinajumuisha "watu wenye afya njema" na "watu wenye haki." Hii haimaanishi kwamba kuna watu ambao hawahitaji Yesu. Hakuna "watu wenye haki," kila mtu anahitaji Yesu. (See: rc://*/ta/man/translate/figs-hypo and Luke 5:31-32)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Maelezo yaliyodokezwa

Katika sehemu kadhaa za sura hii mwandishi alidokezea habari fulani ambayo wasomaji wake wa awali wangeelewa na kuwazia. Wasomaji wa kisasa labda hawajui mambo hayo yote, hivyo wanaweza kuwa na shida kuelewa mambo yote yaliyoandikwa na mwandishi. UDB mara nyingi huonyesha jinsi habari hiyo inaweza kutolewa ili wasomaji wa kisasa waweze kuelewa vifungu hivi. (See: [[rc:///ta/man/translate/translate-unknown]] and [[rc:///ta/man/translate/figs-explicit]])

Matukio ya zamani

Sehemu za sura hii ni mfululizo wa matukio ambayo tayari yametokea. Katika kifungu fulani, wakati mwingine Luka anaandika kana kwamba matukio yamekwisha kutokea wakati matukio mengine bado yanaendelea (ingawa yamekamilika wakati anaandika). Hii inaweza kusababisha shida katika kutafsiri kwa kuunda utaratibu wa matukio usiofaa. Inaweza kuwa muhimu kufanya haya thabiti kwa kuandika kana kwamba matukio yote yamekwisha kutokea.

"Mwana wa Binadamu"

Yesu anajiita mwenyewe kama "Mwana wa Binadamu." Lugha zingine haziwezi kuruhusu mtu kujitaja mwenyewe kama 'mtu wa tatu.' (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/sonofman)

<< | >>